’tulipo, tunakoelekea’ 1 tafakuri ya kila wiki tafakuri ya awali

30/06/2024

Ni rahisi kujitumbukia mshimoni lakini ukiwa umikshaingia shimoni ni vigumu kutoka. Kupanda mlima ni ngumu lakini ukiteleza kuna uwezekano wa kutafuta njia nyingine ya kuendelea kupanda ilimradi una ramani na dira ya kukuongoza. Unapopanda mlima kuna kilele cha kumulika njia. Ukiwa shimoni unakuwa gizani. Huna taa wala ramani ya kukuongoza. Kila mara ukijaribu kutoka unajikuta umepotea.  Unaendelea kuzama zaidi na zaidi. 

Tumekumbatia siasa za kilebarali (liberal politics) na uchumi wa kiulibarali-mamboleo (neoliberal economics). Tulichoelekezwa tumetekeleza. Ramani zetu tumezichanachana. Taa zetu tumezizimazima. Ramani tunaletewa – kwa mkopo. Ikishindwa kufanya kazi tunaiacha. Inakuwa gofu. Mkopo unabaki. Tunaomba mpya. Tunaletewa ya mitumba iliyopigwa rangi. Kuirudisha hatuwezi. Tumefungwa na mkataba. Haya ni mzunguko. Tumenaswa katika mtandao. Tunazunguka humo humo ingawa kila mara tunakuwa na njozi (illusion) ya kupiga hatua. Tunarudi pale pale tulipoanza. Ndio uhalisia wa kuzunguka mtandaoni. 

Tunafikirishwa tuna tajirika kumbe tunafukarika. Ni sawa na mtu anayekimbia juu ya treadmill. Mita inaonyesha ameenda mbali kumbe amebaki pale pale. Ndivyo ilivyo mfumo wa uliberali mambo leo. 

***

Dalili za  mzunguko badala ya maendeleo ni nini? Moja ni mikopo. Tuna aminishwa tunakopesheka. Tunakopa zaidi na zaidi. Mikopo inarundika. Hisa kubwa ya kodi zinazokusanywa kutoka kwa wananchi kila bajeti inaenda kurejesha mikopo. Tunajibana. Tunapunguza bajeti ya afya, elimu, kilimo ilituweze kumudu ulipaji mikopo. Inatubidi kila mwaka tuongeze ushuru na tozo. Wanaoumia ni wananchi wa hali ya chini. Matajiri wana njia chungu nzima kukwepa kodi. 

Chukua mfano wa kodi ya asimilia mbili ya mazao yote ya kilimo iliyoletwa na bajeti ya mwaka huu. Atakaye lipa ni nani? Halipi mfanyabiashara anayenunua mazao. Yeye ama ataongeza bei ya kuuza au ata punguza bei ya kununua mazao au yote mawili. Vyovyote vile atakaye athirika ni mzalishaji (mkulima mdogo) au mnunuzi. 

Kila tukiwa na naksi katika bajeti serikali ama inapandisha kodi au kuongeza mkopo kutoka ndani au nje. Tukikuta mapato ya ndani hayatoshi kurejesha deni inatubidii tukope. Tunakopa kurejesha mikopo ili tuweze kukopa. Tayari tukishaingia kwenye mtego wa deni (debt trap).   

Vyovyote vile hatimaye anaathirika ni mzalishaji wa ndani. Wazalishaji wa ndani wakitozwa kodi kupita kiasi inapunguza uwezo wao wa kulimbikiza mtaji wa kuwekeza. Uwekezaji wa ndani unaathirika.  Tunaendelea kutegemea uwekezaji kutokea nje. Wawekezaji wa nje wanachuma faida lakini faida yenyewe inatoroshwa kuwekezwa katika chumi zilizoendelea. Kwa kifupi, faida inayozalishwa  nchini inawekezwa nje. Matokeo – nchi tajiri zinaendelea kitajarika wakati nchi zinazoendelea kudhoofika. Vilevile nchini tabaka ndogo la madalali linatajirika wakati waliowengi wanafukarika. Hao wanaishi maisha ya kianasa wakati wananchi wana tafuta milo. 

Sasa je hoja inayosema nia na lengo la uwekezaji wa nje ni kupanua sekta za mikakati ili kuongeza ajira na kutanua uchumi? Tutazungumzia hoja hizi katika tafakuri ijayo.

 
*** ***

Leave a comment

Hey!

I’m Bedrock. Discover the ultimate Minetest resource – your go-to guide for expert tutorials, stunning mods, and exclusive stories. Elevate your game with insider knowledge and tips from seasoned Minetest enthusiasts.

Join the club

Stay updated with our latest tips and other news by joining our newsletter.

Categories

Tags