28/07/2024
Maliasili ni ya wote
Kwa matumuzi ya sisi sote.
Maliasili si yangu au yako au ya binamu
Wala shangazi au mjomba
Maliasili ni ya sisi sote.
Maliasili sio kitu cha kuhodhi
Wala mali ya kumiliki.
Maliasili sio bidhaa ya kuyauza
Au kuyapigia bei mnadani
Wala ya kuwekea dhamana mikopo.
Maliasili sio bidhaa ya kubinafsisha
Au kuyagawa kwa wawekezaji.
Au kuyazawadia mwanawe.
Maliasali ni urathi wa wote
Kwa matumizi ya sisi sote.
Ubepari umepora maliasili zetu
Ardhi, madini, mafuta na misitu.
Miito, milima, hewa safi na maji
Yote kwa mabepari ni mali ya kuhodhi.
Kuzalisha faida bila kikomo.
Tukombowe maliasili zetu
Tuzuie uporaji wa maliasili zetu.
Tusitishe ubinafsishaji wa urathi wetu
Tukomeshe uharabifu wa miito na maji yetu.
Turejeshe maliasili kwa umma.
Tusiweke rehani maliasili zetu
Tusichezee hatma ya vizazi vyetu.
Karne tano za uporaji na utesaji inatosha.
Sasa tuamke: tufichue mafisadi na wasaliti
Tuvue nguo wapigadili na wanafiki.
Tumechoka na maneno matamu
Na matendo mabovu.
Tumechoka na wimbo wa maendeleo
Pasipo na utu wala ustawi
Haki wala usawa.
‘Maliasili-ni-ya-sisi-sote’
Kwa matumizi ya pamoja ya jamii zetu
Na vizazi vyetu vijavyo.
Wimbo wetu ni moja, tuimbe pamoja
‘Maliasili-ni-ya-sisi-sote’.
Kaulimbiu yetu ni moja, tuipigie kelele pamoja
‘Maliasili-ni-ya-sisi-sote’.
Dai letu ni moja, tulipiganie kwa nguvu zetu zote
‘Maliasili-ni-ya-sisi-sote’.
*Sing together, act together, fight together:
‘Make Commons a category of common language’.*



Leave a comment